Back to top

News

erikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa onyo kwa wachanjaji au watumishi watakaohusika na kazi ya kutoa chanjo na utambuzi wa mifugo kote nchini watakaojiongoza vibaya na kujaribu kuwatoza wafugaji fedha za afua ya uchanjaji na utambuzi wa mifugo, kinyume na muongozo wa kitaifa uliotengezwa na Wizara kwa kuwashirikisha wadau wote na kisha ukazindiliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya Kitaifa mnamo wa tarehe 16 Juni 2025 Wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu.