Back to top

Makampuni ya ulinzi yasiyofuata sheria yaonywa.

27 June 2020
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ameyataka baadhi ya Makampuni binafsi ya ulinzi kufuata masharti ya vibali walivyopewa na Jeshi hilo pamoja na kufuata maelekezo mengine yanayotolewa huku akiahidi kuvifutia vibali hivyo baadhi ya makampuni ya ulinzi yatakayoshindwa kutekeleza masharti hayo.

IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na wamiliki wa Makampuni binafsi ya ulinzi kwenye kikao kazi cha kujadili utendaji wa makampuni hayo.

Kuhusu suala la usafirishaji wa fedha, IGP Sirro, ameelekeza baadhi ya Makampuni ya ulinzi kuacha tabia ya mazoea ya kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha na badala yake watumie Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa fedha hizo huku watakaoshindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.