
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, ameelekeza kufanyika tathmini ya makampuni yote ya urasimishaji ili kubaini yaliyofanya vizuri na yaliyofanya vibaya yachukuliwe hatua.
Silaa amesema Mhe.Rais ametoa fedha za kutosha na magari, ili wananchi warasimishiwe maeneo yao na wapewe hati lakini baadhi ya makampuni hayakamilishi kazi, hivyo yeye hatosita kuyachukulia hatua yale yaliyofanya vibaya.
Waziri Silaa ameeleza hayo wakati akifunga rasmi Kliniki ya ardhi katika eneo la Bunju wilayani Kinondoni mkoa wa Dar es Saalaam iliyoanza tarehe 19 Februari, 2024.
Pia Silaa amesema makampuni yatakayobainika kusuasua yatasaidiwa kwa kupitiana kubaini changamoto zao na wapi yanahitaji kusaidiwa ili kukamilisha kazi na hatimaye wananchi wapewe hati zao.
