Back to top

MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA MAONESHO YA SIDO NJOMBE

28 October 2023
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango, ametoa wito kwa Taasisi za fedha nchini, kuweka masharti ya mikopo ya upendeleo kwa viwanda vidogo na vya kati, ili kukuza uzalishaji na kuimarisha sekta hiyo.

Makamu wa Rais ametoa wito huo, wakati wa kilele cha Maonesho ya Nne ya Kitaifa ya Shirika la Kuhudumiwa Viwanda Vidogo (SIDO), yaliyofanyika katika uwanja wa sabasaba mkoani Njombe. 

Makamu wa Rais amesema, ni muhimu kushughulikia suala la upatikanaji wa mitaji kwa riba nafuu, ili kuwawezesha wajasiriamali kuweza kuanzisha viwanda vidogo na vya kati.