Back to top

Makamu wa rais azindua chanjo kukinga Saratani ya shingo ya uzazi

10 April 2018
Share

Makamu wa Rais, Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua chanjo ya kukinga Saratani ya mlango wa kizazi  kwa wasichana kuanzia miaka 14 ambayo itatolewa bila malipo na kwa mwaka huu itatolewa kwa wasichana 616,734 hivyo wasichana wanatakiwa  kupata dozi hiyo pindi wanapotimiza umri wa miaka 14 na dozi ya pili itatolewa baada ya miezi 6 baada ya kupata dozi ya kwanza.

"Chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ni salama na imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani. Hivyo Wazazi ma Walezi wenzangu tuwapeleke binti zetu kupata chanjo hii ili kuwakinga na Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa kuwa ndio inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi”, alisema  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu.