Back to top

Makamu wa Rais azindua Sikukuu ya Nanenane Simiyu.

01 August 2020
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua  Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika Viwanja  vya Nyakabindi Mkoani Simiyu leo Agosti 01,2020. 

Ujumbe wa mwaka huu “Nanenane kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Kiongozi Bora 2020”.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Muongozo wa Kitaifa wa Uongezaji wa Virutubisho katika matumizi ya mazao ya Chakula wakati wa  Uzinduzi  wa Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu leo Agosti 01,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi  Muongozo wa Kitaifa wa Uongezaji wa Virutubisho katika matumizi ya mazao ya Chakula Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima mara baada ya kuuzindua Muongozo huo leo Agosti 01,2020  katika  uzinduzi wa Sherehe ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Jengo la Kituo cha Elimu kwa Wakulima Kanda ya Ziwa Mashariki wakati wa Uzinduzi wa Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika leo Agosti 01,2020 Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. ambapo ujumbe wa mwaka huu Nanenane kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Kiongozi Bora 2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia baadhi ya Mazao ya aina mbalimbali ikiwemo Vitunguu maji, Nyanya na Viazi Mviringo alipotembelea mabanda maonesho katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane vya Nyakabindi Mkoani Simiyu leo Agosti 01,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia mazalio ya Samaki alipotembelea Banda ya JKT katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane vya Nyakabindi Mkoani Simiyu leo Agosti 01,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangali Ng'ombe wa Maziwa kwenye mabanda ya maonesho katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane vya Nyakabindi Mkoani Simiyu leo Agosti 01,2020.