Serikali ya mkoa wa Mtwara imesema itaendelea kuwachuja makandarasi wa ujenzi wa barabara ambao ni wababaishaji ambapo kwa mwaka 2019/2020 makandarasi wanne wamebainika kutoa taarifa za uongo kwa wakala wa ujenzi wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) ili kupewa kazi.