Back to top

Makandarasi wazembe na wasiozingatia mikataba ya kazi kuwajibishwa

10 July 2020
Share

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw.Anamringi Macha amewaonya Makandarasi wazembe na wasiozingatia mikataba ya kazi akidai kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha miradi mingi ya maendeleo ya wananchi kujengwa chini ya kiwango ambapo amedai kuwa wote wanaofanya mchezo huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bw.Macha ametoakauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara na madaraja yanayojengwa na makandarasi wazawa katika halmashauri ya Msalala wilayani humo zikiwemo barabara na madaraja  ambayo yamesombwa na kuharibiwa na mafuriko ya maji ya mvua katika msimu wa masika.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara za mjini na vijijni (TARURA) katika halmashauri ya Msalala amesema makandarasi wanaojenga barabara na madaraja hayo wanapaswa kukamilisha kabla ya tarehe 15 mwezi Agosti mwaka huu.