
Makarani waongoza wapiga kura, wametakiwa kuwa waadilifu pamoja na kuzingatia Katiba ya nchi, Sheria za Uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume, wakati wanatimiza majukumu yao.
.
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Zakia M. Abubakar leo Juni 04, 2024, wakati akifungua mafunzo kwa Makarani waongoza Wapiga Kura yatayofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi-Unguja.
.
Mafunzo hayo ni moja maandalizi katika kuelekea uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kwahani, visiwani Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika Juni 08, 2024, ambapo kabla ya ufunguzi huo Makarani hao wapatao 30 walikula kiapo cha kutunza siri na Kujitoa uachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Bi.Safia Iddi Muhammad.
