Back to top

Makonda aungana na Dkt.Mengi kupokea mwili wa Mercy Anna Mengi.

07 November 2018
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda, ameungana na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi, familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kupokea Mwili wa mmoja wa waanzilishi wa Makampuni ya IPP Mama Mercy Anna Mengi. 

Mwili huo umewasili nchini majira ya Saa 9 Alasiri hii leo ukitokea nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika hosptali ya Mediclinic Morningside ya Johannesburg, alifariki tarehe 31/10/2018.

Aidha Mwili wa mama Mercy Anna Mengi unatarajiwa kuagwa hapo kesho baada ya ibada itakayofanyika katika kanisa la Azania Front na kisha kusafirishwa Machame Moshi na kuzikwa siku ya Jumamosi Novemba 10 ,2018.