Back to top

Makonda azindua mfumo kuwabana watendaji wasiotekeleza majukumu yao.

09 October 2019
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw Paul Makonda amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kutoa malalamiko dhidi ya watendaji wasiotekeleza majukumu yao na kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi.

RC Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya "Njoo Kesho" pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM eleza changamoto zako, tuma kwenye namba 11000 na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho. Huduma hii ni bure