Back to top

"Makosa ya jinai yamepungua kwa asilimia 19.1".IGP Sirro

07 April 2021
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema katika kipindi cha miezi mitatu makosa ya jinai yamepungua kwa asllimia 19.1 huku ya usalama barabarani yakipungua kwa asilimia 14 kutokana na weledi wa askari wa Jeshi hilo katika kusimamia sheria.

IGP Sirro amesema hayo leo akiwa kisiwani Zanzibar ambapo amesema licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo makosa ya udhalilishaji na dawa za kulevya pia amewaagiza Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es salaam, Tanga, Pemba pamoja na Unguja kisiwani Zanzibar kufanya operesheni ya pamoja kudhibiti makosa hayo ikiwa pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.