Back to top

Malipo ya TASAF kwa kaya masikini nchini kufanyika Kielektroniki.

10 July 2020
Share

Wananchi wanaonufaika na Mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini nchini (TASAF) awamu ya tatu, sasa wataanza kupokea fedha za mpango huo kwa njia za kielektroniki kwa lengo la kuepusha watu wasiokuwa na sifa kuingia kwenye mpango huo sambamba na kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Afisa Malipo kwa njia ya mtandao kutoka TASAF makao makuu, Zacharia Nyinyimbe ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakuu wa idara kuanzia ngazi ya halmashauri watakaotekeleza kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF ambayo inahusisha vijiji vyote nchini.

Mkuu wa kitengo cha mafunzo kutoka TASAF makao makuu, Mercy Mandawa amesema watekelezaji wa mpango huo wa TASAF katika kipindi hiki cha pili cha awamu ya tatu ni lazima wahusika waapishwe ili watakapokwenda kinyume na malengo ya mpango huo waweze kuwajibishwa.