Back to top

MALORI 25 YAKWAMA MGOLOLO WILAYA YA MUFINDI IRINGA

04 April 2024
Share

Zaidi ya magari ya mizigo 25 ambayo yanasafirisha bidhaa mbalimbali kutoka kiwanda cha karatasi Mgololo Wilaya Mufindi mkoani Iringa, yamekwamba kwa zaidi ya siku tano katikati ya Vijiji vya Nyamande na Kitandiliko Halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe kutokana na ubovu wa barabara katika eneo hilo.

Madereva wa magari hayo akiwemo Godwin Ngajilo na Jumanne Hussen wamesema changamoto kubwa katika eneo hilo inatokana na aina ya kifusikisicho na changarawe kilichowekwa na mkandarasi ambacho kimesababisha Barabara hiyo kutopitika kutokana na uwingi wa matope kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Madereva hao wamesema kutokana na adha hiyo kumesababisha watumie gharama kubwa kwa ajili ya kupata chakula na kueleza kuwa mpaka sasa hakuna jitihada zinazoendelea kwaajili ya kunusuru hali hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu Meneja wa Tanroad mkoa wa Iringa, Yudas Msangi, amekiri kupokea changamoto hiyo na kuahidi kutafutia ufumbuzi haraka na kueleza kuwa barabara hiyo itafanyiwa marekebisho.