Back to top

Mama Samia asisitiza Watanzania wasiache kufanya mazoezi. 

09 August 2020
Share

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kwa watanzania kutokuacha kufanya mazoezi kwani mazoezi ni muhimu kwa afya.

Makamu wa Rais Mhe. Samia amesema hayo leo asubuhi Agosti 09,2020 baada ya kumaliza mazoezi ya kutembea masafa ya kilomita nne yaliyoanzia kwenye Makazi yake Mtaa wa Farahani ulioko  Kilimani Jijini Dodoma.