Back to top

MANING NICE YAFELI BREKI MILIMA YA USAMBARA

03 July 2023
Share

Abiria zaidi ya 60, walioukuwa wakisafiri kutoka wilayani Lushoto, kwenda mkoani Dar es Salaam kwa kutumia basi la kampuni ya Maning Nice, lenye namba za usajili T 122 DEA, wamenusurika kifo baada ya breki za basi hilo, kushindwa kufanya kazi kwenye mteremko mkali wa milima ya Usambara, mkoani Tanga.
.
ITV imezungumza na dereva wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la Twariki Abdallah, ambaye amesema kuwa gari hilo liliishiwa upepo, hivyo aliamua kuliingiza kwenye gema, ili kuepuka madhara zaidi.