
Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma imesitisha uchinjaji wa nguruwe katika maeneo yote ya Manispaa hiyo,kufuatia kuibuka kwa homa ya nguruwe ambayo haina kinga wala tiba.
Takwimu ambazo zimetolewa na Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Songea, Bwana BilalY MWEGENI zinaonesha kuwa homa ya nguruwe katika kipindi cha kuanzia Januari hadi tarehe 14 mwezi huu imeua nguruwe 864.
Hata hivyo amesema takwimu hizo za vifo ni matukio ambayo yameripotiwa katika Idara yake,lakini uchunguzi umebaini kuwa zaidi ya nusu ya nguruwe wali o po Songea wamekufa kutokana na ugonjwa huo.
Amesema takwimu zinaonesha kuwa Manispaa ya Songea ina nguruwe 4,581na sensa ya idadi ya nguruwe waliobakia katika Manispaa ya Songea inakadiriwa watakuwa hawazidi Elfu-Mbili ,kwa sababu kuna nguruwe wengi wamekufa na takwimu za vifo haz ijafikishwa rasimi ofisini kwake.