Mkoa wa Manyara umetajwa kushika nafasi ya pili kwa matukio mengi ya ukatili wa kijinsia jambo ambapo wakazi wa mkoa huo wametakiwa kutumia madawati ya Jinsia ili kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Makongoro Nyerere wakati wa uzinduzi wa Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi cha Orkesment Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Jamii Faustine Shilogile amesema kwa sasa wameendelea kupeleka Wakaguzi wa kata katika maeneo mbalimbali nchini ili waweze kusaidia katika kupunguza uhalifu ikiwemo vitendo vya ukatili wa
kijinsia.
Kwa upande wake Msaidizi wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu na Afya ya uzazi (UNFPA) Dkt. Majaliwa Marwa amesema wamesaidia ujenzi wa ofisi hiyo ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.
