
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, ameagiza Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) cha Mutukula, Bw. Feisal Nassoro na wenzake watatu ambao ni Bw. Gerald Mabula, Bw. George Mwakitalu na Bw. Emmanuel Malima ambao ni maafisa mapato wa TRA warudishwe makao makuu mara moja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu ya kudharau mamlaka na na kuikosesha Serikali mapato.
“Mkuu wa Wilaya ni mkuu na msimamizi wa shughuli za Serikali ndani ya wilaya yake. Anapotaka taarifa anastahili apatiwe. Uongozi wa mkoa ulipokuja nao pia waliambulia dharau. Hatuwezi kukubali kuona mtumishi wa umma anafanya mambo ya hovyo halafu sisi tunamuacha,” Waziri Mkuu
Ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wakazi wa Mutukula, mara ya kufanya ukaguzi kwenye Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani (One Stop Border Post) cha Mutukula, wilayani Missenyi mkoani Kagera.