Back to top

MAOMBI YA PALSTINA KUANZISHA KITUO CHA MICHEZO TANZANIA

19 October 2023
Share

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt.Damas Ndumbaro , amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Tanzania Mhe.Hamdi Mansour Abuali, Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Mhe.Ndumbaro, amepokea maombi ya nchi ya Palestina kupitia Balozi huyo, kuanzisha Kituo cha Michezo Jijini Dar es Salaam na kuahidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Mhe.Balozi Hamdi amewasilisha ombi hilo akieleza kuwa, nchi hiyo ina ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo Utamaduni na Michezo, hivyo Kituo hicho kitakua na umuhimu kwa nchi mbili hizo katika kukuza michezo.