
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom, amependekeza upanuzi wa utoaji wa chanjo ya Malaria duniani.
Tedros Adhanom amesema Shirika la Afya Duniani linapendekeza chanjo ya pili iitwayo R21/Matrix-M itumike, ili kuzuia Malaria kwa watoto walio katika hatari ya ugonjwa huo.
Amesema ushahidi unaonesha kuwa katika maeneo ambayo maambukizi ni ya msimu, Malaria hupungua kwa sabini na tano baada ya dozi tatu za chanjo ndani ya miezi kumi na miwili.
