Back to top

MAREKANI YAITAKA SENEGAL KUFANYA UCHAGUZI HARAKA IWEZEKANAYO

14 February 2024
Share

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Senegal Macky Sall, ambapo amemtaka kuhakikisha uchaguzi nchini humo unafanyika haraka iwezekanavyo, ambapo amesisitiza kuwa angependa kuona uchaguzi huo unafanyika katika tarehe iliyopangwa ambayo ni Februari 25, 2024.
.  
Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Matthew Miller, amesema, Marekani ina wasiwasi mkubwa na Taifa hilo kutokana na kusogezwa mbele kwa uchaguzi wake hali ambayo imesababisha mzozo wa kisiasa nchini humo.
.
Ikumbukwe jana Februari 13, 2024, Mamlaka nchini Senegal zilizuia mawasiliano ya simu pamoja na intaneti ili kudhibiti maandamano yenye lengo kupinga uamuzi wa Serikali ya nchi hiyo kusogeza mbele uchaguzi.                          #via #DWSwahili