Back to top

Marekani yaweka kigingi mazungumzo na Korea Kaskazini.

21 August 2019
Share

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema Marekani haijarejea katika meza ya mazungumzo na Korea kaskazini kama ilivyotarajia.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha matangazo cha CBS Pompeo ameongeza kwamba Marekani ilifahamu kwamba mazungumzo hayo yangekuwa magumu.

Alipoulizwa iwapo Marekani ina wasi wasi juu ya makombora ya masafa mafupi yanayofyatuliwa na utawala wa Korea kaskazini, Pompeo amesema ndio na kuongeza kwamba angependelea utawala huo kutofanya hivyo.

Wakati huo huo Pompeo amekiri leo kuwa wanamgambo wa Dola la Kiislamu wanapata nguvu katika baadhi ya maeneo lakini amesema uwezo wa wanamgambo wa kundi hilo wa kufanya mashambulio umepungua.

Pompeo amesema kuna maeneo ambako kundi la ISIS lina nguvu hivi leo kuliko ilivyokuwa miaka mitatu ama minne iliyopita.