Back to top

Marufuku H/Mashauri kupima viwanja kwa kutumia Makampuni binafsi.

11 August 2020
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi amezipiga marufuku halmashauri nchini kupima viwanja kwa kutumia makampuni binafsi na badala yake kazi hiyo ifanywe na watalaam wa ardhi wa halmashauri.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo wakati akizindua ofisi za ardhi za mkoa wa Ruvuma ambayo itatoa huduma ya hati za ardhi kwa wananchi badala ya kufuata hati zao ofisi ya ardhi kanda ya kusini mkoani Mtwara.

Tazama Video Hapa