Back to top

MARUFUKU KUINGIZA MAGARI MABOVU BARABARANI

03 April 2024
Share


Madereva mkoani Songwe, wametakiwa kuacha tabia ya kuendesha magari mabovu kimazoea ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao na kuleta madhara kwa watumiaji wengine wa barabara.

Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassoro Sisiwayah, Mkuu wa operesheni kikosi cha usalama barabarani alipofanya ukaguzi katika kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto kilichopo Chimbuya mkoani Songwe

ACP Sisiwayah amesema dereva anatakiwa kujali usalama wake kwanza kisha kuwajali watumiaji wengine wa barabara ili kuweza kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuepukika.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Songwe, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Charles Bukombe amewataka madereva kutii sheria bila shuruti na sio kushtukizwa na operesheni kama hizi.