
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Awadhi Juma Haji amepiga marufuku tabia iliyolalamikiwa na waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda ya baadhi ya Askari wa kikosi cha usalama barabarani kupokea fedha taslimu ya faini wanayowatoza wandesha Bodaboda hao wanapowakamata kwa makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa kanuni na sheria za usalama barabarani.
