Marufuku luninga za hospitali kuonyesha burudani.

Naibu Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Dk Faustine Ndugulile amewataka waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanza kutekeleza maelekezo ya serikali yanayoagiza  luninga zote zilizofungwa kwenye hospitali za umma kurusha matangazo yanayohusu vipindi vya elimu ya afya peke yake.
 
Dk Ndugulile anatoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua changamoto zinazowakabili wagonjwa katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo anasema lengo la serikali kuweka luninga hizo ni kutoa elimu ya afya na si tamthilia michezo na burudani kama ilivyozoeleka.