Back to top

MARUFUKU UUZAJI NYAMA UGANDA, KISA KIMETA

11 March 2024
Share

Kutokana na kuwepo kwa Ugonjwa wa Kimeta nchini Uganda, Serikali nchini humo imepiga marufuku uuzaji wa Nyama katika mji mkuu, Kampala, pamoja na kuamuru kufungwa kwa maeneo yote ya kuchinja ili kupunguza kuenea kwa mlipuko huo. 

Serikali licha ya kupiga marufuku uuzaji wa Nyama kutokana na Ugonjwa huo, lakini pia ilitaka endapo nyama itauzwa wanyama wapimwe kabla ya kuchinjwa, jambo ambalo pia wafanyabiashara nchini humo wamepinga marufuku hiyo na kuishutumu serikali kwa kushindwa kudhibiti ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Kimeta umeripotiwa katika Wilaya 40 kote nchini Uganda, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.