Back to top

Mashirika ya ndege ya Nigeria yasitisha mgomo.

09 May 2022
Share

Mashirika ya ndege ya Nigeria yamesema kuwa yamesitisha mpango wa kugoma kutoa huduma za usafiri wa ndege za ndani uliokuwa uanze  Jumatatu wenye lengo la kupinga ongezeko la gharama ya mafuta ya anga.

Waendeshaji wa Mashirika ya Ndege ya Nigeria (AON) wamesema bei imeongezeka karibu mara nne mwaka huu, ambayo haikuwa endelevu lakini wamesema  wataendelea na safari za ndege wakati mazungumzo na serikali yakiendelea.