Back to top

Masomo ya sayansi yatakaiwa kufundishwa kwa vitendo

18 September 2019
Share

Ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda walimu wa masomo ya sayansi wametakiwa kuwajengea uwezo wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu pamoja na kuwafundisha kwa vitendo kuanzia elimu ya msingi na sekondari.

Ili kuleta ufanisi katika kuwafanya wanafunzi kuelewa na kuyapenda masomo hayo Mradi wa Mammie Chini ya Shirika la SHIPO Unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la We Weld umeanza kutoa mafunzo ya siku tisa  kwa walimu wa masomo ya sayansi kutoka kata tatu za wilaya ya ludewa Mkoani Njombe ili kuboresha  mbinu za ufundishaji ili kuzalisha watalamu wa sayansi wa hapo badae.

Kwa upande wao wakufunzi wa Masomo ya Sayansi Toka Chuo Cha Ualimu Vikindu mkoani Pwani akiwemo Ester Richard anasema jamii haipaswi kendelea kuogopa masomo ya Sayansi kama ambavyo wameaminishwa kwani Tanzania ya viwanda haiwezi kufikiwa bila kuwa na wataalamu wa Sayansi na teknolojia.

Walimu wa masomo ya sayansi na hesabu kutoka shule za msingi za kata za Mawengi ,Milo, Mlangali na Lubonde wilayani Ludewa wamesema kuwa baadhi ya mada zinakosa ufanisi katika ufundishaji kutokana na kukosa baadhi ya vifaa vinavyohitajika katika mafunzo kwa vitendo ambapo wameiomba serikali kuendelea kuajiri walimu wa masomo ya sayansi kwa kuwa waliopo hawatoshelezi.