Back to top

Matapeli mtandaoni TAMISEMI yatoa tahadhari.

13 January 2022
Share

Wizara ya TAMISEMI imetoa tahadhari kwa wadau wake na wananchi wote juu ya uwepo wa wahalifu wa mitandaoni wanaotumia jina la Waziri wa TAMISEMI Mh. Innocent Bashungwa kutapeli watu huku wakibainisha namba zinazotumiwa na wahalifu hao ni 0692-483200 na 0692-483290 ambapo wizara hiyo imesema kuwa tayari imewasiliana na Mamlaka husika kwa hatua za kisheria dhidi ya wahalifu hao.