Back to top

Matarajio ya Bajeti 2020/2021.

11 June 2020
Share

MACHACHE KUELEKEA BAJETI KUU YA SERIKALI YA 2020/2021

Waziri wa fedha na mipango Dkt.Philip Mpango amesema mpango uliopo kaatika bajeti ya mwaka 2020/21,  msukumo mkubwa utawekwa katika kukarabati miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha nchini na kukamilisha utekelezaji wa miradi inayoendelea kwa lengo la kupata matokeo tarajiwa ikijumuisha kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ili kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kuchochea uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu.

Kuhusu Mfumuko wa bei Waziri Mpango amesema umeendelea kupungua na kufikia asilimia 3.2 Mei 2020, kutoka asilimia 3.5 Mei 2019 kutokana na kuimarika kwa ugavi wa chakula nchini na kupungua kwa bei za nishati ya mafuta katika soko la dunia na mpango ni kuendelea Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki katika wigo wa tarakimu moja kati ya wastani wa asilimia 3 hadi 5 kwa mwaka 2020/21.

Kwa upande wa deni la serikali Mhe.Mpango Amesema hadi kufikia Aprili 2020, deni la Serikali lilifikia shilingi trilioni 55.43 ambalo imechangiwa na kupokelewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na kusisitiza deni bado ni himilivu.

Muda mchache ujao Hii Waziri wa Fedha Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Tizama Uchambuzi kutoka kwa Dkt.Ngowi akiwa na Mtangazaji Isakwissa Mwaifuge, uweze kufahamu mengi tukisubiria Bajeti kusomwa hapo baadae.