Back to top

MATATANI KWA KUDANGANYA KUUZA FIMBO YA MALKIA

10 January 2024
Share

Mahakama ya Southampton nchini Uingereza imemkuta na hatia ya ulaghai, Dru Marshall mwenye umri miaka 26, mkazi wa Hampshire kusini mwa Uingereza, baada ya kijana huyo kutangaza kupitia ebay, kuuza kile alichodai kuwa ni fimbo (mkongojo) iliyokuwa ikitumiwa na Malkia Elizabeth II.
.
Imeelezwa kuwa Kijana alitengeneza mnada wa kuuza fimbo hiyo, kupitia ebay na kusema kuwa yeye ni moja ya wafanyakazi katika Kasri la Windsor, na mapato yatakayopatikana baada ya kuuza fimbo hiyo yangeenda kwenye utafiti wa magonjwa ya saratani na kwamba tayari mnada huo ulikuwa umefikia pauni 540 sawa na Tsh. 1,728,338/=, kabla hajausitisha baada ya kugundua kuwa anafuatiliwa na Polisi.