
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP. Isack Mushi amesema Jeshi hilo linawashikilia watu 20 mkoani humo, baada ya kukutwa na viuatilifu mbalimbali vyenye ruzuku ya Serikali kinyume cha sheria ambapo amebainisha kwamba walifanikiwa kuwakamata watu hao kupitia taarifa fiche ndipo Jeshi hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) lilianza operesheni ya pamoja kuwasaka watuhumiwa hao.
