
Bw.Samwel Maikut (60) mkazi wa Kitawio huko nchini Uganda,amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kwenda ukweni mikono mitupu, kwa ajili ya sherehe ya utambulisho bila mahari.
Baba mkwe wa Samwel Bw.Christopher Ngania amesema kama familia walijipanga kupokea wageni kwa ajili ya shughuli lakini walishtuka baada ya ugeni huo kuwasili ukiwa mikono mitupu.
Na bwana harusi huyo alitakiwa kwenda na ng'ombe wanne, mbuzi watatu, pamoja na vitu vingine lakini walikuja watupu.
Mzee Maikut amekubali kuwajibika kwa kila kilichotokea kuwakasirisha wakwe zake ikiwemo kulipa gharama za shughuli zote, ambapo pia atawalipa shilingi milioni 3 za Uganda wake zake kabla ya Disemba 30.
Kwa mujibu wa kiongozi wa ukoo wa Bwana harusi,inasemekana kuwa bwana harusi hakuwashirikisha ukoo katika maandalizi yake , hivyo hawakuwa wanajua kuhusu masuala ya kupeleka ng'ombe.
