Back to top

Matokeo ya Simba yamkatisha tamaa Mo Dewji aamua kujiuzulu.

13 January 2020
Share

Baada ya timu ya Simba kupoteza mchezo wa fainali ya #MAPINDUZICUP2020 , Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohammed Dewji ametangaza kujiuzulu nafasi yake katika bodi na kubaki kama mwekezaji.

"Inakatisha tamaa kuona Simba haijashinda. Baada ya kulipa mishahara ya karibu Bilioni 4 kwa mwaka. Ninajiuzulu nafasi ya  Mwenyekiti wa bodi na nitabaki kama Mwekezaji. Simba Nguvu moja. Nitaelekeza nguvu kukuza miundombinu na kukuza vipaji kwa vijana". MO DEWJI.