Back to top

Matukio 22 ya mauaji ndani ya mwezi mmoja

18 January 2022
Share

Waziri wa Mambo Ndani Mh. Hamad Masauni amesema katika kipindi cha kuanzia Januari 1 hadi 15 mwaka huu jumla ya matukio 22 ya mauaji yanayohusisha ndugu wa familia moja na wivu wa kimapenzi yameripotiwa kutokea nchini ambapo amewataka viongozi wa dini nchini kuisaidia serikali kuwaelimisha wananchi kuwa na hofu ya Mungu.