Back to top

Mavunde aagiza kampuni ya Five Star kufikishwa Mahakamani.

12 July 2018
Share

Naibu waziri wa Kazi Vijana na Ajira Mh.Anthony Mavunde ameagiza kampuni ya Five Star inayojishughulisha na kazi ya kuchapisha nyaraka mbalimbali kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kuajiri raia wa nje bila ya kuwa na vibali sambamba na  wafanyakazi waliokutwa na kosa hilo nao kufikishwa Mahakani mara moja. 

Mbali na agizo hilo pia Mh.Mavunde ameaagiza kiwanda hicho kulipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 20
Kutokana na kukutwa na makosa mbalimbali ikiwemo uchafu.

Kiongozi huyo amefikia hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafula kiwandani hapo kwa lengo la kubaini
Utendaji kazi wake na ambapo alijionea hali ilivyo sambamba na wafanyakzi kumweleza kero zao.

Hata hivyo viongozi wa kiwanda hicho walipoulizwa kuhusu mapungufu ya kiwanda hicho na hasa kuwa
Wafanayakzi bila vibali, mikatana hawakuwa na majibu ya kutosha kamishina wa kazi kuagiza ndani ya siku
14 mikataba mipya iandaliwe na ifikishwe wizarani.