Back to top

Mawaziri wateule pamoja na Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali kuapishwa

13 September 2021
Share

Mawaziri wateule pamoja na Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali walioteuliwa jana  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan watakula viapo leo katika Ikulu iliyopo Chamwino  mkoani Dodoma.

Wanaotarajiwa kula kiapo hicho ni Mh.Dr.Stergomena Tax ambaye atakuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mh.Dr.Ashatu ambaye atakuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Wengine ni Mh.January Makamba ambaye atakula kiapo kuwa Waziri wa Nishati na Mhe.Profesa Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi huku Dr.Eliezer Feleshi akitarajiwa kula kiapo cha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mh.Makamba, Mh.Mbarawa  na Mhe.Kijaji wanachukua nafasi za  Mh.Dr.Medard Kalemani, Mh.Dr.Faustine Ndugulile na Mh.Leornard Chamuriho ambao teuzi zao zimetenguliwa.

Naye Dr.Feleshi anachukua nafasi ya Profesa Adelaus Kilangi ambaye ameteuliwa kuwa balozi ilhali Dr.Tax anachukua nafasi ya Marehemu  Elias Kwandikwa aliyefariki wiki chache zilizopita.