Back to top

Mawaziri wawili wafika Mtwara kutatua mgomo wa madereva wa Dangote.

19 April 2021
Share

Mawaziri 2 wa viwanda na biashara Prof.Kitila Mkumbo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji Gofrey Mwambe wamewasili mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja na kutembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kwa dhamira ya kutatua mgomo wa madereva ulioingia siku ya 12 leo.
.
Mawaziri hao wamewasili kwenye kiwanda hicho na kupokewa na uongozi wa kiwanda hicho ukiongozwa mtendaji mkuu wa kiwanda Bw.Abdullah Baba.