
Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta, imetembelea maeneo ya hifadhi na chanzo cha maji katika mkoa wa Katavi, kujionea hali ya uvamizi wa maeneo hayo ,ambapo imeelekeza wananchi waliovamia maeneo hayo kutofanya maendelezo, mpaka hapo timu ya wataalamu itakapokamilisha kazi yake kuhusiana na mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye maeneo hayo.
Kamati hiyo inayohusisha Wizara nane za kisekta, imetembelea eneo la hifadhi la mito miwili lilipo kitongoji cha Kasekese wilayani Tanganyika pamoja na chanzo cha maji cha Milala kilichopo kata ya Misunkumilo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Kiongozi wa Kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika ziara hiyo Mhe.Mashimba Ndaki amewaeleza wananchi wa Kisekese kuwa, uamuzi wa mwisho kama eneo hilo liendelee kuwa hiadhi au maeneo ya kuishi watu itajulikana baada ya kupata majibu kutoka kwa wataalamu.
