
Aliyekuwa mwakilishi wa ITV/Radio One mkoani Dodoma, Shaban Tolle, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana, katika hospitali ya Mama Ngoma, Dar es Salaam, anatarajiwa kuzikwa leo baada ya Swala ya Alasiri kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Marehemu utatokea Msikti wa Manyema Kariakoo ambako utaswaliwa na kupelekwa Makaburi ya Kisutu kwa maziko.
Shaban Tolle alifariki dunia kwa maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali Pema Amina.

