Back to top

Mbaroni kwa kuiba mtoto mchanga wa jirani yake.

28 April 2021
Share

Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia Bi.Angelina Masumbuko mkazi wa kata ya Bugurula mkoani Geita kwa tuhuma za kuiba mtoto mwenye umri wa wiki mbili nyumbani kwa jirani yake wakati mama yake akiwa amelala kisha kutokemea pasipojulikana.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Henry Mwaibambe anasema baada ya kufanya msako mkali wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa amemficha mtoto huyo mchanga.