Jeshi la polisi mkoani Arusha limekamata jumla ya watuhumiwa 9 wakiwemo vijana wawili wakiwa wanatumia jina la Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof Florence Luoga kufanya utapeli wa kuwaibia watu kwa njia ya Mtandao.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Jonathan Shana amesema katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa ushirikiano wa askari wa wanyamapori kutoka TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro pia wamekamata Bunduki mbili za kivita risasi 15,majangili wawili wakiwa na nyama ya twiga na wengine watano wakiwa na meno mawili ya Tembo.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na mashine ya kusajili line za Simu iliyokuwa inatumiwa na vijana hao Juma Husein na Aman Gabriel wanadaiwa pia kutumia hati ya kusafiria ya raia mmoja wa Australia kufanya utapeli huo.