Back to top

Mbaroni kwa kukutwa na vipande kumi vya meno ya tembo Ruvuma.

26 January 2021
Share

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watuhumiwa watatu ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi kwa kukutwa na vipande kumi vya meno ya tembo yenye uzito wa kilo 20. 


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa anasema kukamatwa kwa meno hayo ya tembo kunaonyesha ujangili bado upo licha ya juhudi za kupambana na tatizo  hilo kuendelea kufanywa.