
Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Latifa Bakari mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne baada ya kumpiga. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam,Muliro Jumanne Muliro, amesema baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa mtoto na kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side Ubungo.
