
Mbunge wa upinzani nchini Uturuki, amefariki siku ya Alhamisi, zikiwa ni siku mbili zimepita tangu apate mshtuko wa moyo, na kuanguka mbele ya bunge alipokuwa akimalizia hotuba ya kuikosoa sera ya serikali kuhusu Israel.
Hasan Bitmez, 54, Mbunge kutoka Chama cha Upinzani cha Felicity (Saadet), amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jiji la Ankara, Waziri wa Afya Fahrettin Koca amethibitisha hilo wakati akiongea na waandishi wa habari kwa njia ya televisheni.

Matangazo rasmi ya Bunge yalionyesha Bitmez akianguka chini baada ya kusimama kwenye jukwaa kabla ya mkutano mkuu Jumanne.
