Back to top

Mbunge na familia yake wanusurika kifo.

27 March 2022
Share

Mbunge wa Masasi mjini,  mkoani Mtwara, Geoffrey Mwambe na familia yake  wamenusurika kifo baada ya gari lake walilokuwa wakisafiria  kuungua moto na kuteketea, akiwa njiani kutokea Dar es Salam kuelekea wilayani Masasi kwenye msiba wa baba yake mzazi .

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita mchana katika eneo la Mkwajuni wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa ya  kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi na  Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi, chanzo cha ajali hiyo kimebainika kuwa ni hitilafu  katika mfumo wa umeme ndani ya gari hilo.

Kamanda Kitinkwi amesema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Dionis Aloyce Mwihumbo na katika ajali hiyo ya moto hakuna madhara kwa waliokuwepo ndani ya gari hilo.