Back to top

Mchinja Ng'ombe Mkuu atumbuliwa kwa kuhalalisha nyama ya Kibudu.

23 January 2021
Share

Mkaguzi Mkuu wa nyama wa Manispaa ya Shinyanga Verani Mwaluko amemsimamisha kazi mchinja Ng'ombe mkuu wa machinjio ya manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma ya kuruhusu kuingizwa ndani ya eneo la machinjio nyama ya ng'ombe wawili wanaodhaniwa wamekufa (Kibudu).

Amesema mchinja ng'ombe huyo ali halalisha nyama hiyo ikauzwe kwenye mabucha ya nyama mitaani hali ambayo inadaiwa kuwa ingeweza kuleta madhara ya magonjwa kwa wananchi wa manispaa hiyo.