Back to top

Meya Dar ang'olewa,vurugu zaibuka.

09 January 2020
Share

Kikao maalum cha baraza la jiji la Dar es Salaam kimemwondoa kwenye nafasi yake Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita kutokana na tuhumu zilizokuwa zinamkabili.

Awali kabla ya maamuzi hayo mzozo uliibuka  katika kikao maalum cha baraza la madiwani jijini Dar es Salaam baada ya wajumbe wa upinzani kudai CCM wamegushi saini ya  mjumbe ambaye hayupo kwenye kikao.

Ni baada ya kuwasilishwa kwa taarifa juu ya tuhuma zinazomkabili Meya wa jiji la Dar es Salaam Mstahiki Isaya Mwita.

Baada ya maamuzi hayo Isaya Mwita amepinga maamuzi yaliyotolewa na mkutano uliomwondoa madarakani.